Sababu 8 za Wanaume Kutokuwa Waaminifu Katika Mahusiano Yao ya Mapenzi

Suala la wanandoa kutokuwa waaminifu kwenye mahusiano yao ni suala mtambuka na limekuwa likiongelewa sana na watu wengi. Sababu mablimbali zimekuwa zikitajwa kuwa chanzo, nyingine ni za kweli na nyingine ni zakufikirika tu.

Leo nimeamua kuja na sababu zinazotokana na tafiti za wanaume kutokuwa waaminifu kwenye mahusiano na ndoa. Ikumbukwe kwamba sababu za wanawake kutokuwa waaminifu hazifanani moja kwa moja na sababu za wanaume, na hata kitendo chakutokuwa mwaminifu kwenye ndoa kwa mume au mke pia huathiri ndoa husika katika uzito tofauti. Hii ni kutokana na sababu za kiasilia, kiuumbaji, kijinsia na kisaikolojia.

Sababu:

1. Utupu au upweke ndani ya moyo wa mwanaume

Pamoja na kwamba wanaume huonekana wakiwa jasiri sana kwa nje ila ieleweke kwamba ni viumbe dhaifu ndani, ni viumbe wasioweza kuvumilia upweke ndani yao, wakati wote hutamani kuwa karibu na mwanamke hata kama akiwepo karibu hawaelewani mara kwa mara. Maranyingi kwenye mahusiano unakuta mwanaume ameoa au ana mpenzi na kuna mambo yanaendelea ambayo yanasumbua mahusiano yao, ukaribu unapokosekama mwanaume huanza kujihisi upweke ndani yake na hapo inanyanyuka kiu ya kutafuta mtu wakuondoa upweke ule.

Inasemekana kwamba wanaume wengi huchepuka au kuanza mchakato wa kuchepuka kunapokuwa na tafrani kwenye mapenzi au ndoa, ni kwanini? Sababu ni kwamba ule ugomvi umeleta baridi moyoni na nafsini kwa mwanaume na hawezi kustahimili upweke huo ndani yake kwahiyo anatafuta faraja haraka sana.

Ndio maana tafiti zinaonyesha mara nyingi kwamba mke anapofiwa na mumewe, mke anaweza kuishi muda mrefu bila ya mume na asiolewe, ila mume hawezi kuishi muda mrefu bila kuoa na wale wanaoishi bila mke tena maranyingi hufariki sio muda mrefu.

Ndio maana ulimwengu una wajane wengi kuliko wagane (wanaume waliopoteza wake zao). Ili kupunguza athari za mwanaume kutokuwa mwaminifu ninashauri wanandoa kuhakikisha ukaribu baina yao “intimacy” ni mkubwa na wanaukoleza kwa makusudi kila mara ili kuiepusha ndoa yao kuingia kwenye misukosuko ya kukosekana kwa uaminifu “cheating”

2. Uasili wa kiu kubwa ya mwanaume katika tendo la ndoa

Kiaasili na kibaiolojia mwanaume anakiu kubwa na utayari wa kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, mwanaume wa kawaida anaweza kutamani kufanya tendo la ndoa hata kila siku, na wengine hata marambili kwa siku kama kila kitu akilini na katika afya yake ni sawa. Utayari na uwezo huu ni tofauti sana kulinganisha na wanawake ambao kama akifanya tendo zuri la ndoa na hamu yake ikitoshelezwa basi anaweza kukaa muda fulani bila kutamani tena.

Mwanaume hajaumbwa hivyo na wala hawezi. Kwa bahati mbaya kwenye ndoa nyingi wanandoa hawafundishwi haya kwahiyo hawafahamiani asili zao, mwanamke anadhania kuwa atafanya tendo la ndoa anavyotamani yeye kumbe mume aliyenaye ni kiumbe mwingine wa tofauti sana anatamani kupewa tendo hilo kila mara, kwa kutokutosheka mwanaume analazimika kupenya kwenye kona nyinginezo na kupata anachotamani.

Kwa ndoa ya kawaida, mwanamke analazimika kufanya tendo landoa katika nyakati anazotamani na kujisikia na hata zile ambazo atafanya tu ili kumfurahisha na kumsaidia mumewe kufurahi na ndio maana kuna tendo la ndoa la aina mbili kwenye ndoa, tendo la ndoa wakati wote mnafuraha na hamasa na mnajisikia “pleasure s3x” na tendo la ndoa wakati mmoja au wote hamko kwenye hamasa lakini mnalazimika kufanya kwasababu ya uhitaji wa mmoja au usalama wa ndoa yenu “duty s3x”.

3. Kubadilika kwa uzuri, urembo na maumbile ya mke

Mara nyingi ninapoongea na wanawake huwa ninawaambia kwamba mume wako anakupenda uwe vile alivyokupenda alipokutana nawewe, mabadiliko yoyote ya ziada kutoka kwenye ile hali iliyompa hamasa awali yanaweza kuigharimu ndoa yako. Wanaume ni watu wenye kuhamaki au kuwa makini kwenye umbo, umbile na muonekano wa mpenzi wake kwasababu kwa asili mwanaume huvutiwa zaidi na akionacho, mwanaume hufungulia milango ya hisia inayohusu tendo la ndoa kupitia anachokiona zaidi kuliko vitu vingine vyote.

Wanaume wengi waliohojiwa wameripoti mwamba wamepoteza mvuto kwa wake zao kwasababu wake hao wameongezeka maumbo, wamekuwa wanene sana, tumbo limeongezeka, kiuno kimeongezeka, wengine wamesema kwamba uzito na ukubwa wa mwili unawafanya wanawake hawa kutokuwajibika ipasavyo wanapokuwa kitandani, mume anaona kama anadhulumiwa, anakosa ile hamasa aliyoizoea kwenye tendo la ndoa, anakosa ule ushirikiano na uwajibikaji aliouzoea na anaoupenda.

Kumbuka kwamba tendo la ndoa ndio kitovu cha furaha ya mwanaume kwahiyo mabadiliko yoyote yanayoathiri tendo hilo ni hatari sana kwake. Ushauri wangu kwa wanawake, msidharau hoja za waume zenu kuhusu miili yenu, ukisikia anakwambia fanya mazoezi, au anakwambia umeongezeka sana, tafadhali sana zingatia na wala usichukie wala kuhamaki au kuhisi kuwa anatania, kwake huo ni ujumbe muhimu sana. Na wale ambao waume zenu ni wakimya na hawaongei basi fahamu kuwa ndani yake kunakitu kinasugua akili kuhusu kuongezeka kwako, jaribu kufanya kitu kukusaidia kurudi ulivyokuwa awali. Yeye anapenda na inamfurahisha hata kama hasemi.

4. Kuchangamkia fursa ya kupata tendo la ndoa jepesi

Kwasababu wanaume ni watu wanaopenda tendo la ndoa mara kwa mara, na kwasababu wake zao hawako tayari kutimiza kiu hii mara kwa mara kulingana na uhitaji, wanaume wengi huchangamkia fursa pale wanapokutana na uwezekano wakupata tendo la ndoa kirahisi na kiwepesi.

Hii huongezeka zaidi pale ambapo kuna misuguano ndani ya nyumba na kwahiyo wanandoa hawawezi kuweka hisia na mawazo yao katika tendo la ndoa, mume hatakama anakiu kiasi gani anawaza anamuanzaje mkewe, maana anajua fika kwamba atakataliwa, wengine kutokana na ukaribu “intimacy” baina yao kuwa mbaya, mwanaume anaona ugumu kumtongoza mkewe ampe tendo la ndoa, akiwaza kuanza mchakato huu anaona nijukumu zito kama kujenga nyumba, sasa mtu wa hivi anapopata fursa rahisi na nyepesi kutoka kwa kiumbe yeyote wa kike ukweli ni kwamba hatoiacha.

Hapa ndipo panapochochea biashara ya umalaya, kwasababu mwanaume anaona ngoja nitumie shilingi elfu tano au kumi au ishirini ilimalizane nahii hamu maramoja nirudi nyumbani. Ndio maana pia wanawake waliorahisi au wanaojirahisisha kingono hutumiwa sana na wanaume hususani na waume za watu maana kiu yao ni kuitumia fursa hiyo kiufasaha na kuondoka “no strings attached”.

5. Kisasi “revenge”

Mara nyingi wanaume hutumia kitendo cha kutoka nje ya ndoa au nje ya mahusiano kama fimbo ya kulipiza kisasi kwa maumivu au hasira yoyote aliyokuwa nayo dhidi ya mpenzi au mke wake. Kwa mfano, wanaume wengi nilioongea nao binafsi, hususani wale ambao walikuwa wanalalamika kuwa mke wangu haniheshimu, mke wangu ananidharau, mke wangu hanisikilizi, mke wangu anafanya hivi au anafanya vile, wengi baada ya kuongea au kulalamika kwa muda mrefu pasipo kuona mabadiliko baadaye waliamua kuanza ku “cheat”.
Kisaikolojia, mwanaume anapochepuka kwa sababu ya kisasi, huwa inamwondolea ile hali ya kujishtaki au kushtakiwa nafsini kwamba amefanya kosa “guilty conscious” na hiyo inaweza kumfanya aendelee kuchepuka kwa muda mrefu tu, tofauti na mwanamke anapochepuka.

Ni vema ukachukua tahadhari hii, pale unapoona mume wako analalamika sana kuwa haumuheshimu, unamdharau, haumsikilizi, haushuki au kunyenyekea basi fahamu kwamba kunauwezekano mkubwa ameshaanza kuchepuka au yuko kwenye kuisoma ramani ili aanze. Kama kunauwezekano wa kubadili tabia na kushuhulikia hayo malalamiko yake ni bora ukafanya hivyo maana kifuatacho chaweza kuhatarisha mahusiano yenu.

6. Mkanganyiko wa matarajio ya mwanaume

Wako wanaume wengi ambao kabla hawajaoa walikuwa na shauku kubwa kwa wake zao, walikuwa na matamanio au matarajio makubwa kwa wake zao. Wengine walioa wake zao kwasababu ya maumbo mazuri na yakuvutia, wengine ni aina ya familia wanawake hao walizotoka, wengine walioa wakitegemea huyu mwanamke ni mcha Mungu sana, au uliwahi kusikia habari zake nzuri kwa watu na ukatamani sana kuwa naye maishani na mara baada ya kuingia kwenye ndoa bahati mbaya yale mambo uliyokuwa unakiu nayo sana na kuyatarajia unakuta sio yalivyo. Wapo ambao nimeongea nao sana, wanasema walipooa lile umbo zuri sana la mke wake alidhania ndio ustadi wa kitandani baadaye akakuta ujuzi wa tendo la ndoa ni mdogo kuliko matarajio ya mwanaume.

Wengine baada ya ndoa wamekuja kugundua tabia zilizojificha kwa mke ambazo hawakuzijua awali, wengine wameibua madhaifu kedekede kwa wake zao ambayo mwanzoni hawakuyafikiria. Hii hali ya matarajio ya mwanaume kufukiwa na uhalisia huua kabisa hamasa ya tendo la ndoa na hapo inakuwa rahisi mwanaume kuanza kutafuta mahusiano mengine nje.

 7. Kutokupevuka

Wapo wanaume kwenye ndoa hususani wenye umri usio mkubwa sana wamekuwa wakiripotiwa kuchepuka mara kwamara kwasababu tubado hawajafahamu umuhimu wa ndoa ili kuithamini, wameoa lakini bado fikra zao zinatawaliwa na marafiki, hawawezi kujisimamia wenyewe, mtu anaweza kukaa baa na marafiki hadi usiku sana bila kujali kwamba ana mke na watoto. Huko nje usiku ndipo fursa za uchepukaji huzaliwa. Wapo ambao wamechelewa kupevuka kutokana na aina ya malezi waliyolelewa na wazazi wao “spoilt children”, hawa hushindwa kuiheshimu ndoa na mke hatakama mke alalamike vipi.

Kila siku kesi ni kuhusu michepuko, simu imekutwa na picha za ngono za mwanamke, simu ina ujumbe wa mapenzi na vingine vingi vinavyofanana na hivi. Baadhi ya ndoa za wanaume wa hivi zimevunjika mapema kwasababu wake zao walishindwa kustahimili. Kupevuka hakuangalii sana umri, mwanaume anaweza kuwa na umri wa miaka 40 lakini bado haonyeshi kupevuka. Kupevuka ni kukua au kupanuka kwa uwezo wa kufikiri hususani katika kuithamini na kuiheshimu familia, mke  na ndoa kwa ujumla.

8. Kujifariji kwamba kila mtu anafanya

Wapo wanaume wengi walioonyesha kuchepuka kwasababu tu ndani yao walikuwa wanakosa umaana wa kuwa waaminifu kwasababu wanaona hata wale watu ambao wao waliwaamini kwamba labda wanaweza kutochepuka na wao pia walichepuka, sasa mtu anasema kumbe kila mwanaume anachepuka, basi yanini kujibanabana wakati namimi ninahamu na fursa inaruhusu.

Kile kitendo chakuona wanaume wengi wanatabia ya kutokuwa waaminifu kudhoofisha mioyo ya wanaume wengine kwa kujifariji kwamba kumbe hichikitu sio kipya, kila mtu anakijua na anafanya, chakujitahidi tu ni kutokugundulika. Pamoja na hayo wito wangu kwa wanaume wenye fikra hizi ni kwamba, kuwa kwako mwaminifu kwa ndoa yako hakutakiwi kuyumbishwa na tabia za wengine, usimtegemee mtu kukutengenezea misingi ya uaminifu wa ndoa yako, je kama kila mwanaume anampiga mke wake na wewe ndio uanze kumpiga? Kama kila familia inaugomvi, na wewe ndio utafute ugomvi hata kama hakuna mazingira ya ugomvi? La hasha!!

Ifahamike kwamba, haijalishi ni sababu gani imemfanya mwanaume au mwanamke kuchepuka au kukosa uaminifu katika ndoa yake, madhara ya tabia hii yanaweza kuigharimu ndoa yako kwa kiasi kikubwa sana. Madhara yake yanaweza pia yasiishie kwenu ninyi wanandoa tu bali yakawaathiri hata watoto wenu. Wito wangu ni kila mwanandoa kuithamini na kuiheshimu ndoa yake kutoka ndani yamoyo na sio kinafiki.

JE, WAJUA SEHEMU ZINAZOMPA UTAMU MWANAMKE ? SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

Kwa bahati nzuri wanawake wana maeneo 5 ambayo huwawezesha kusikia utamu wa kufanya ngono tofauti na wanaume. Sehemu maarufu ni kisimi na G spot lakini kuna eneo lingine linaitwa AFE ambalo liko mwishoni kabisa mwa uke na vile vile kuta za uke bila kusahau mwanzo wa uke.

Mwanamke huweza kupata utamu wa tendo hili takatifu kwenye maeneo yote hayo ikiwa mpenzi wake anajua kuwajibika, sio kufanya mapenzi kwa muda mrefu tu bali pia kujua kucheza na uume wake. Pamoja na utundu wake pia wewe mwanamke unatakiwa kuwa wazi na huru kumuelekeza ikiwa kagusa kusiko au kapatia kunako utamu. Utamu wa maeneo yote hayo ni tofauti na unazidiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine.

Hebu sasa tutazame hizo sehemu tofauti za utamu wa ngono kwa wanawake.

Kisimi Wanawake hupata utamu wa kisimini kwa njia ya kusuguliwa, kushikwa, kuchezewa kwa ulimi, kidole au kichwa cha uume. Utamu wa mahali hapa hupatikana haraka na hufanya usitamani tena tendo hilo kwa muda fulani (Kuanzia dakika 3 – 15) na kikiguswa tena huweza kumpa mwanamke maumivu fulani hivi. Baadhi ya wanawake huwa hawawezi kuendelea

tena na tendo mara baada ya kuchezewa

kisimi. G-spot Utamu wa mahali hapa ni wa nguvu sana na wanawake wengi huishiwa nguvukwa muda wanapoguswa eneo hili. Nguvu hizo huchukua muda wa dakika 20 – 45 kurejea, na zikirejea hamu haiishi. Hivyo wakati wewe umezimia mpenzi wako anaweza kuendelea na mchezo na nguvu zikirudi basi na wewe unaendelea kutafuta goli lingine.

Mwanzo wa uke Utamu wa mahali hapa haumpotezei mwanamke hamu, kwani hafiki kileleni bali anasikia utamu fulani hivi. Ili mwanamke aweze kufika kileleni,mwanaume anatakiwa aingize uume ndani zaidi ili aweze kugusa eneo la G- Spot na kuta za uke.

Kuta za uke Utamu wa eneo hili unapatikana toka mwanzo uume ulipoingizwa, na kadri mnavyoendelea kufanyana ndivyo utamu unavyozidi kuongezeka na hatimaye mwanamke hujikuta akifika kileleni. Mwisho wa uke (karibu na njia ya uzazi) Utamu wa eneo hili hupatikana endapo uume wa mpenzi wako utagusa mwisho wa uke. Kwa kawaida mwanamke husikia maumivu flani anapoguswa eneo hili lakini wakati huo huo badoanapenaendelee na wakati mwingine anaweza kumuomba mpenzi wake afanye kwa nguvu. Pia mwanamke anaweza kutokwa na damu endapo ataguswa eneo hilo. Ewe mwanamke,hakikisha unamruhusu mpenzi wako kufika huko ikiwa mnaaminiana, mko kwenye uhusiano wa kudumu, msafi kiafya na uko tayari kuwa mama endapo mpenzi wako atateleza na kuachia kidogo kwani eneo hili lipo mlangoni kabisa mwa njia ya uzazi.

FAHAMU WANAUME HUPENDA KUOA MWANAMKE WA AINA HII

Habari za wiki hii mpenzi msomaji. Mimi namshukuru Mungu kwa kuweza kunikutanisha na nyinyi kupitia safu hii ambayo pamoja na mambo mengine nazungumzia juu ya mada mbalimbali ambazo zinagusa maisha yetu ya kila siku.Wiki hii nitazungumazia juu ya aina ya wanawake ambao wanaume wengi hupendelea kuoa. Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa

MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.

Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.

WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya. Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.

WENYE UCHU NA MAENDELEO

Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani ‘golikipa’. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini. Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

WASIOPENDA MAKUU

Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia “leo tunakwenda wapi dear?” Akimuona rafiki yake kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia, “mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.

Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana uwezekano haupo.

WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?

Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.

Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini Dar-es-Salaam. Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.

Je umajua Upendo wa Mapenzi unahitaji vitu vya aina gani????

Asante sana kwa kuendelea kutembelea kutufwatilia siku ya  leo tunataka kuzungumza na wewe mambo muhimu yatakoyokufanya uweze kudumu katika mahusiano.,Ili uweze kudumu katika masuala ya mahusiano ya kimapenzi ni lazima ujue ya kwamba ipo haja ya kujua mambo haya yatakayokusaidia wewe kudumu katika mahusiao hayo.

1. Imani
Upendo unahitaji imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasio onekana unatakiwa kuwa na imani na mwenzi wako imani katika mausiano ni muhimu sana kuaminiana toa wasiwasi kwa mwenzi wako mwamini kuwa amekuchagua wewe hakuna mwingine ukopeke yako.

2. Ujasiri
Upendo unahitaji uwe jasiri katika hali zote uajasiri katika kunena ujasiri kutenda, ujasiri katika kuuzungumzia upendo kwa mwenzi wako upendo unamhitaji mtu jasiri sio kitu rahisi kama wengine wanavyozungumzia.

3. Mawasiliano
Upendo unahitaji mawasiliano maana mawasiliano hutengeneza mahusiano bila mawasiliano huku na mahusiano ili ujenge msingi mzuri mzuri wa mahusiano yako unahitaji uwe mtu mzuri katika mawasiliano- mawasiliano yana uwezo mkubwa sana wa kutunza mahusiano hivyo upendo unahitaji mawasiliano.

4. Asante
Upendo unahitaji neno asante kwa mwenzi wako kwa lolote atakalo litenda kwako kama atakupa zawadi asante hasa kwa mpenzi wako ni neno muhimu sana na linaongeza nguvu ya mapendo uwe unatumia neno hili asante kwa mpenzi wako maana upendo unahitaji neno hili ASANTE. Hata baada ya kutoka katika tendo la ndoa sema asante maana ni tendo la ndoa ni matokeo ya mapendo. Hivyo upendo unahitaji ASANTE.

5. Haki
Upendo unahitaji haki unatakiwa umtendee haki mwenzi wako usimyime haki yake ya msingi kumtunza kumpenda na kumtimizia haki zake zote najua unajua haki za mapenzi wako- upendo ili ukomae unahitaji haki iwapo katika mahusiano yenu.

BODA BODA VS CHANGUDOA

Kazi yake ya bodaboda, uaminifu, ustaarabu na upole aliokuwa nao kwa wateja wake ndiyo hasa uliomfanya Joakim kuwa na wateja wengi sana katika eneo lake la kazi (Kijiwe kama wengi wanavyoita), lililopo Sinza Makaburini jijini Dar.

Wafanyakazi, wanafunzi, wafanyabiashara na wengineo wanaoishi maeneo hayo ya

jirani walipenda sana kumtumia Joakim katika shughuli zao mbalimbali kama kuwabebea mizigo yao na kuwapelekea nyumbani hata kwenye mishemishe zao za kila siku, jina lake likafahamika na kuwa maarufu sana miongoni mwa wafanyabiashara ya usafiri wa pikipiki maaruku kama ‘bodaboda,’na kujikua akibadilishwa jina na wateja wake kutoka Joakim na kufupishwa kwa kuitwa Kim.

Ugumu wa maisha ndiyo ambao ulipelekea Kim kutoroka kijini kwao Mkoani Morogoro na kukimbilia jijini Dar ili kujikwamua katika ugumu wa maisha aliokabiliana kama ilivyo kwa Watanzania wengi. Alipofika jijini haku na ndugu yeyote wala jamaa jambo lililopelekea miezi kadhaa kulala katika Kituo cha Mabasi yaenda Mikoani cha Ubungo, na hatimaye akawa maarufu sana kituoni hasa kutokana na kujishughulisha kazi ya kubeba mzigo ya abiria kama wafanyavyo vijana wengine.

Aliendela na kazi hiyo kwa uamini kwa sababu ni sehemu ya talanta yake aliyozaliwa nayo, na aliaminika zaidi na hata baadhi ya vijana wenzake na hata viongozi wa kituo hicho, hasa katika kufanya kazi na kupata hesa ya

halali kuliko kumtendea mabaya binadamu mwingine.

Maisha yalizidi kusonga na akiendelea na kazi ya ukuli kwa kubeba mizigo ya abiria wanaoingia kwa wingi na kutoka Kituo cha Ubungo kila siku.

Baada ya kukaa kwa muda mrefu akifanya kazi ya ukuli akabaini ili aweze kukabiliana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli inabidi afikirie namna ya kujikwamua au kufanya kazi nyingine ambayo itamsaidi maisha yake. Kitu cha kwanza harakaharaka alichokifikiria kukifanya ni kujifunza udereva kwani elimu yake ya darasa la nne ndiyo ilimpa shaka sana ya kupata kazi nyingine.

Alijipinda kwa miezi sita akipigana huku na kule kuhakikisha amepata shilingi laki moja ambayo itamsaidia kulima hela kwa mmoja wa madereva wa pikipiki ili amfundishe lakini pia hela ile imsaidie katika matumizi yake ya kila siku. Hatmaye Kim alifanikiwa kutunza  kiasi cha pesa alichokihitaji na ndipo hapo alipopata nguvu ya kwenda kwa Yule dereva wa pikipiki aliyekuwa anamfikiria na kuongea naye kuhusu kumfundisha kuendesha.

Kwa kuwa hakuwa anatania alifika na kuongea naye kasha akatoa noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi yule dereva wa pikipiki na kumwambia anaomba awe anamfundisha kuendesha kama yeye, jamaa alikubali kwa haraka na kumuona Kim kama mtu aliyejua shida yake ya siku hiyo kwani pamoja na siku kuwa inaelekea kuisha hakuwa amekamilisha hesabu ya bosi wake jambo lililokuwa linamuumiza sana akili na kufikiria mtu wa kumkopa ilimradi tu akamilishe hesabu ya bosi wake.

Walipanga siku na muda wa kuanza kujifunza namna ya kuendesha pikipiki na hatimaye baada ya mwenzi mmoja Kim akawa amefahamu kuendesha pikipiki na kuifanya roho yake kuwa na shauku ya kupata pikipiki ya kuendesha kama njia moja wapo ya kufanya biashara na ikiwezekana aache kabisa pale Ubungo.

Haikuwa kazi ngumu sana kwa Kim kupata pikipiki kwani yuleyule mwalimu wake wa kuendesha ndiye aliyemsaidia kupata pikipiki kwa kumuunganisha na mmoja wa mama ambaye alikuwa amenunu pikipiki mbili baada ya kupata kiinua mgongo chake. Mama Yule alipomuona Kim alivutiwa naye na nkumuamini kasha akampa pikipiki yake kwa sharti la kuitunza na kuipenda kama yak wake.

Ni Alfajiri ya Jumatatu Kim aaliamaka kwenda kwa mama mwenye pikipiki na kuichukua kasha kuelekea nayo katika kijiwe kilichopo Sinza Makaburini na kupaki pikipiki yake mpya kwa ajili ya kusubiri wateja kama wafanyavyo wenzake, baada ya wiki, mwezi na hatimaye miezi Kim alikuwa kishafahamika sana na kuwa na wateja kibao wa kuwasafirisha sehemu mbalimba za Jiji la Dar.

Ni mwaka sasa umekatika Kim  akiwa amefanikiwa kuwa na geto lake nzuri lenye godolo moja, kitivi cha kiaina ba baadhi vyombo vya kuwekea maji pindi anaporudi kutoka kwenye mizunguko yake. Akiwa bado yuko eneo lake la kazi akijiandaa kuondoka ghafla akatokea msichana mmoja mzuri sana kimuonekano lakini alikuwa amevaa nusu uchi, wakati Kim akiendelea kumshangaa mrembo yule, akazidi kushangaa zaidi kuona mrembo yule anazidi kumsogelea. Wakati huo ilikuwa ni majira ya saa 3 usiku, wenzake wakiwa wameishatawanyika makwao.

Je, mrembo yule atakuwa ni nani? na anataka nini kwa Kim?

Na M&U

Fahamu dalili/ ishara za mchumba mwenye mapenzi ya kweli

– Anakuheshimu na anakufanyia mambo yote kwa heshima

– Muda wote uko kichwani kwake/anakuwaza wewe.

– Anakusikiliza na anafanya unachokisema

 – Anaweza kukushika bila kuogopa watu. mfano, mkono mkiwa sehemu zenye watu wengi

– Anakujali.

– Anataka uipende na ushirikiane na familia na ndugu zake –

– Anaweza kuomba msamaha

– Akiwa anaongea badala ya kusema nita…. anasema tuta…. mfano, tutafanya hivi badala ya nitafanya hivi

– Anakuweka kwenye mipango yake ya baadae

–  Anasema ‘SASA’. (Mfano SASA tufanyeje?) Anatumia neno sasa kukupa nafasi ya kutoa mawazo yako

Fahamu Hizi Hapa ni Aina 7 Ya Vyakula Vinavyoongeza Nguvu za Kiume.

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia “booster”. Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.

 Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
  • Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
  • Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
  • Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume

Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.
1. Blueberry
Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi
2. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.
3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.
4. Karanga
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.
5. Vitunguu saumu
Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.
6. Ndizi
Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).
7. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.

Chukua Elimu ya Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Katika Ndoa ili idumu……

Wapenzi wasomaji wa Jitambue Kwanza, hakuna asiyependa kufurahia utamu wa ndoa katika maisha yake yote ya ndoa. Leo ninakukumbusha tu baadhi ya vitu vitakavyokufanya uishi katika ndoa yenye furaha na upendo siku zote.

1. SIRI – Ukiwa katika ndoa, siri ni kitu muhimu sana ambacho huenda ukikifuata kitakuepusha na mambo mbali mbali yatakayosababisha ndoa yako iteteleke. Chagua watu maalumu unaowaamini ili uwatumie katika kuomba ushauri kwamfano, wataalamu wa mambo ya ndoa au saikolojia, ndugu wa karibu au rafiki yako wa karibu sana, na wale wote unaowaamini. Ukifanya hivyo utawaepuka wale wote wenye nia mbaya na ndoa yenu.

2. KUWA MUWAZI KWA MWENZIO – Binadamu tumeumbwa tofauti tofauti, huenda kitabia pia tukawa hatujakamilika kuweza kumudu hali tofauti tofauti zinazotukabili katika maisha yetu, lakini yote hayo mwisho wa matatizo ni kuwa muwazi, kwani wahenga walisema; mficha maradhi kifo humuumbua. Mweleze mwenzi wako pale alipokosea ili ajirekebishe, kuliko kukaa kimia rohoni bila kusema.

3.JIFUNZE KUOMBA MSAMAHA UNAPOKOSA – Hakuna suluhu nzuri na nzito kama kuomba msamaha pale unapokuwa umekosa, maana ukithubutu kufanya hivyo kwa mwanadamu mwenzio, hata kwa Mungu utasamehewa. Jishushe pale mwenzio anapokuwa na ghadhabu juu yako, pengine unaweza kuwa hujakosa, lakini kushuka kwako kunaweza kukamfanya mwenzio ajutie kosa endapo kweli kama atakuwa amekosa. Lakini pia endapo ukijua wewe ndiye mwenye makosa, basi omba msamaha ili kuokoa muda.

4. MCHUKULIE MWENZI WAKO KAMA PACHA WAKO – Mara nyingi umri wa wanandoa hutofautiana sana au kidogo, lakini unapokuwa tayari katika ndoa, vipengele hivi hupotea. Ni vizuri ukamheshimu mkeo au mumeo kwasababu ya ndoa yenu na sio kigezo tu cha umri. Kuna baadhi ya wanaume kuwachukulia wake zao kama watoto na kutoa amri mbaya hata mbele ya watoto wao, hupaswi kufanya hivyo, kwani huo utakuwa ni unyanyasaji wa kijinsia.

5. KUWA MSAFI  – Unapoamua kuwa msafi, sio kuishia katika nguo na mwili wako tu, bali hata kwa watoto wenu pia. Hakikisha nguo za familia zinakuwa safi, na sio kurundika nguo chafu ndani kwa wiki nzima au kuloweka nguo wiki nzima. Uzuri wa nyumba ni pamoja na usafi.

6. MTUMAINI MUUMBA WAKO NA MEMA UTAYALA – Ndoa yoyote ile inayomcha Mwenyezi Mungu, itadumu hadi mwisho wa maisha yao. Wanandoa mnapaswa kumuhofu Mungu wakati wote, kwani mkifanya hivyo mtazibwa macho ya usariti, kiburi, michepuko na hata matamanio yaletayo magonjwa katika ndoa au familia yenu.

TAMBUA MWANZO MWA UTAMU WA MAPENZI NA DALILI ZAKE

Nimshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na kuweza kuikamilisha siku salama bila kupata tatizo lolote kubwa, ni jambo la kumshukur nawe mwana-M&U Kwa kukuepusha na balaa mbalimbali kwa siku ya leo.

Karibu sana katika kuelimishana juu ya maisha ya kawaida na yale ya mapenzi ambayo yanawasumbua na kuwaliza wanadamu bila kujali, cheo, rangi, umri, wadhifa, elimu au dini, wayu wengu hulia, huteswa kwa ajili ya mapenzi kila kukicha duniani kote.

Mada ya leo inazungumzia MWANZO MWA UTAMU WA MAPENZI AU MAPENZI MATAMU-MWANZO
Najua umeipenda sana hii mada ili kuweza kujua utamu ambao unazungumzwa na M&U ni upi , hapa nazungumzia kuwa mara nyingi mapenzi huwa ni matamu pindi yanapoanza.
Huwa matamu kwa sababu ya vitu kadhaa ambavyo vinakuwa miongoni mwa wahusika yaani wapenzi.

Kwa kuwa mila na tamaduni za Kiafrika mwanaume ndiye ambaye anapaswa kumtongoza mwanamke basi hapo ndipo tunapoanzia, kwani mwanaume anapokuwa anamtongoza mwanamke au binti fulani kuna mambo kadhaa huyafanya au hufanyika;

MUDA
Kwa mwanaume anayeanza kutongoza, kutumia muda wake kwa ajili ya mwanamke anayemtongoza, si tatizo kwake hata kama atakuwa amebanwa na kazi kwa namna gani yuko radhi kudanganya au kumuua hata mtu (kusingizia msiba), ilimradi apate muda wa kwenda tu akamuone mpenzi wake.

UMBALI WA ENEO

Utamu mwingine utauona pale ambalo pamoja na kuwa na umbali wa kimakazi kati ya mwanaume na mwanamke lakini bado mwanaume anafunga safari na kwenda kumuona mpenzi wake na pengine inaweza kuwa hata kila siku iendayo kwa MUNGU. Na anafanya hivyo kwa sababu ya NGUVU NA UTAMU WA MAPENZI.

MAWASILIANO
Hata suala la kuwasiliana na mwanamke huyo huwa ni la lazima, mara kwa mara iwe kwa kumpigia simu, kumtumia ujumbe mfupi wa maneno au kuonana naye.
Kitendo hicho cha mawasiliano wapenzi wengi hasa wanawake wanapenda sana kuwa na mawasilianao ya mara kwa mara na mpenzi wake.

Kupitia mawasiliano hayo mwanaume atakuwa anamuuliza mpenzi wake mara kadhaa, “vipi babu umeishakula, unakula nini leo, ratiba yako leo ikoje mpenzi wangu, natamani tuishi wote ili uwe unanichagulia nguo za kuvaa na kadhalika” vitu ambavyo wanawake wanapenda sana, wanapenda kujuliana hali mara kwa mara na huo ndiyo utamu wa mapenzi kwa mwanzoni.

ZAWADI
Kwa mwanamke kwake huwa ni matamu sana wakati anatongozwa kwani mwanaume ataonesha kila aina ya kujali, kuwasiliana na hata kutoa zawadi mbalimbali kama maua, kadi, nguo za ndani, vocha, Muvi, sirizi na zinginezo ili mradi tu kuonesha kuwa anajali hata kama hana hulka hiyo.
Hata hivyo kwenye zawadi wapenzi huwa wanatofautiana kuna wengine bila zawadi wanaona kama hawapendwi ila kuna wengine kwao kawaida, umpe, usimpe ni yaleyale.

Mapenzi matamu bhana! Hiki ndicho ambacho unaweza kujibu kama utauliza ni nini kitamu zaidi katika maisha ya mwanadamu.
Utamu huo wa mapenzi ufikia ukingoni pindi wapenzi wanapozoeana na kuanza kudharaulia hapo ndipo migororo na mikasa mambalimbali huanza kuibuka na hata wengine kutengana kwa muda au mazima kabisa. Wakati mwingine viongzi wa dini na hata wazee wa koo wa pande pili wanaweza kuingilia kati kwa ajili ya kunuthuru ndoa hiyo lakini walengwa wanakuwa wamechokana na kukaa kurudisha penzi lao pamoja na kuwekewa vikao vya familia.

 

DALILI KUMI ZA MAPENZI KUNYAUKA NA KUANZA KUISHA TAARATIBU

Wapenzi wengi ambao wamefikia hatua ya kuachana wameshindwa katika vipimo vya kitalaamu kuthibitisha ubaya waliokoseana, ambao unaweza kubeba uamuzi huo mzito wa kuvunja ahadi zao za kimapenzi na hata ndoa.

Kwa mujibu wa watalaam wa masuala ya ndoa na mapenzi inaelezwa kwamba wapenzi wanaoachana huwa hawana sababu za msingi, hii inatokana na ukweli kwamba wanaoachana hawafahamu kiini kilichowatenganisha katika makubaliano muhimu na ya kwanza kabisa ulimwengu ya watu kufikia hatua ya kupeana utu wao.

Inasemwa hivyo kwa sababu ukilinganisha matatizo yanayotenganisha watu hayabebi hoja zinazokubalika na wapenzi wote. Kwa mfano kama wapenzi watasema wameachana kwa sababu wamefunaniana na wakadhani hiyo ni sababu wanakuwa wanaudanganya zaidi umma kwa maana kuna wanaofumaniana, wanaodhalilishana, wanaotukanana, wasioheshimiana kabisa, lakini bado wanadumu katika ndoa zao bila kuachana.

Kwa ulinganifu huo, wachunguzi wa mambo ya ndoa wanasema, kuachana si zao linaloota na kukua kwa siku moja, bali ni migogoro isiyoshughulikiwa kwa muda mrefu ambayo huwaachanisha wanandoa taratibu bila wao kujua.

Kwa maana hiyo wanaoachana au watakaoachana wanatakiwa kufahamu kuwa safari yao ya talaka haianzi na kumalizika kwa siku moja, isipokuwa hufikia katika hitimisho baada ya kuwepo katika mwendo kwa muda mrefu, ambapo dalili zake huwa hizi zifuatazo:

1 : Ikiwa mmeoana na baadaye mkaanza kuonana ni watu msiohitajiana sana katika maisha. (mapenzi kuchuja). Kila mtu anafahamu kuwa wakati wa uchumba mapenzi huwa moto moto lakini baada ya kuoana hujitokeza hali ya kuanza kuzoea. Hii inatokana na ukaribu ambao mwanzo haukuwepo au kusitishwa kwa machimbezo yaliyokuwa yakiboresha uhusiano. Kwa mfano wapenzi wengi wanapokuwa kwenye uchumba hufanyiana mambo mengi yakiwemo ya kutumiana zawadi na kadi au kutoka pamoja kwa matembezi, lakini wakioana hujikuta hawafanyiani hayo, jambo ambalo huathiri mapenzi yao.

Uchuchuzi unaonyesha kuwa wapenzi walio kwenye uchumba wanapokuwa pamoja hutumia muda mwingi sana kuomngea kwa simu, kutumiana meseji, kuzungumza tofauti na mume na mke. Ukitaka kuthibitisha keti barabarani ukiona mwanaume na mwanamke wamo ndani ya gari hawaishi kucheka na kuzungumza wafuatilie utakuta mwisho wa safari yao wanaagana kila mmoja anakwenda kwake (ina maana si mume na mke hao). Ni nadra sana kuwakuta wanaume wakiwa pamoja na familia zao wakifurahi, jambo ambalo hupunguza upendo na kuleta mazoea na hisia za kutohitajiana sana. Hili halifai likiwepo ni ishara kuwa mapenzi yanakaribia kunyauka.

2 : Mkiwa hamsameheani na kusahau mnapokoseana. Si watu wengi ambao wako tayari kusamehe na kusahau makosa. Wapenzi wa dunia ya leo wakisema nimekusamehe haina maana wamefuta kosa bali hiliweka kando na kulikumbushia wakati mwingine. ‘Hili ni kosa la tatu tarehe fulani ulinifanyia hivi, wiki iliyopita na jana kulinijibu hivi hivi sasa leo siwezi kukuvumilia”
Kauli kama hizi hutoka kwenye vivywa wa watu ambao hawako tayari kusamehe, kosa la mwaka juzi litakumbushwa tena na tena na kuzidi kuchochea ugomvi hata uliokuwa mdogo na kuoneka mkubwa kwa sababu tu umehusishwa na makosa yaliyopita. Inashauriwa kuwa uhai wa mapenzi lazima uambatana na kusameheana kama wanadamu na kusahau makosa. Hili lisipofanyika ni rahisi kuua penzi na kuwafanya watu kuachana. Ni vema kila mmoja wetu akajichunguza tabia yake na kuacha kukumbusha makosa yaliyopita.

3 : Msipokubali kuwekeana mipaka ya kiutawala. Kuna suala linatambulishwa sana siku hizi na wanaharakati, linaitwa usawa wa kijinsia, jambo hili limekuwa likichangia sana migogoro ya ndoa hasa baada ya kutumiwa vibaya na wahusika. Hakuna ubishi mila za kiafrika zinaongozwa na mfumo dume, kuubadili mfumo huu kwa haraka kumekuwa kukiharibu uhusiano mwingi wa kimapenzi kutokana na ukweli kwamba ni wanaume wachache sana ambo wako tayari kuishi na wanawake wanaovutana nao kimamlaka.

Hivyo ili kunusuru hili lisiwe kikwazo katika mapenzi tunashauri kila mwanandoa kuheshimu mipaka yake na kujali zaidi utu na si usawa kama inavyotambulishwa (haya ni mawazo yangu). Watu wanaojali utu katika familia watakuwa tayari kuwapa heshima wanaoishi nao kwa kusikiliza mawazo yao na kutokutumia nguvu kuwakandamiza wengine. Ni vema mwanamke akachungua nafasi yake kwa mumewe na mume naye akamuheshimu mke kwa utu wake.

4 : Msipozungumzia vikwazo vya maisha.

Matarajio ya watu wengi wanapokuingia katika uhusiano wa kimapenzi huwa ni kupata faraja, ni wachache kati yao hufikiria kukutana na vikwazo vya kimaisha. Tafiti zinaonyesha kuwa wakati mtu anapotafuta mpenzi huamini toka moyoni kuwa akiwa na waridi wake matatizo ya upweke, kukosa msaada wa hili na lile yatakwisha lakini baadaye anakuja kubaini kuwa aliyokusudia kuyapata hayapati tena na hivyo kujuta kwa kauli kama hizi. “Kama ningejua kama mwanaume mwenyewe yuko hivi nisingekubali kuolewa.”

Kauli kama hizi mara nyingi hutokea kwa watu ambao hawazungumzii matatizo na vikwazo wanavyokutana navyo katika mapenzi na kuviondoa. Kama mpenzi wako ana matatizo unasubiri nini kuyatafutia ufumbuzi au kama maisha hayaendi sawa ukimya wa nini kwa mwenza wako, kaeni chini muambizane kuwa mnaupungufu wa fedha na dhiki kadhaa wa kadhaa, ili kama kutatokea kukosa mahitaji muhimu liwe ni jambo linaloeleweka na wote kuwa linatokana na kipato kushuka. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wengi wanapokukwama kiuchumi hupunguza matumizi kimya kimya jambo ambalo huwafanya wanawake wengi kubaki wakitumikia zana potofu kuwa huenda wananyimwa baada ya kuwepo kwa nyumba ndogo.

5 : Msipokuwa na mipango ya pamoja na uwazi wa matumizi ya pesa.

Nina ushahidi wa kutosha juu ya kuwepo kwa wapenzi hasa wenye kipato kutokuwa wawazi katika mipango yao ya kimaisha na matumizi yao pesa. Natambua baada ya kufanya uchunguzi wangu kuwa pesa za baadhi ya wanawake huwa hazina matumizi ya wazi, badala yake wanaume hubanwa kwa kisingizio kuwa wao ndiyo wana wajibu wa kutunza familia.
Hali hii imekuwa ikileta migogoro mingi sana kwenye familia na kushusha upendo kwa vile upande unaohudumia familia hapa haijalishi mume au mke huwa unajikuta ukikereka kwa kukosa msaada wa upande wa pili na hivyo kuondoa mapenzi ya kweli. Kama hilo halitoshi vijana wengi wa kiume siku hizi wamejikuta wakiahirisha mapenzi yao kwa wasichana baada ya kukosa ushirikiano wa kimapato na matumizi yake.

“Ninashida ya kuonana na wewe mpenzi wangu, vipi nikufuate kazini?” Jibu linakuwa “Hapana niko bize sana leo.” Inawezekana kabisa mtu akawa hayuko bize lakini kwa sababu anaogopa kukamuliwa kipato na yeye mambo yake hayako sawa anaamua kukacha ahadi. Lakini ukiwepo ushirikiano wa kimatumizi husaidia kudumisha mapenzi.
Inashauriwa kwamba kama wapenzi wote wana kazi na wanapokea mishahara ni vema vipato vyao vyote vikatumika katika kutunza na kuendeleza familia. Tabia ya mwanamke kumtegemea mwanamume kimatumizi huku yeye akitumia pesa zake kwa manunuzi ya vipodozi na nguo au kufanyia mambo yake kwa siri haijengi badala yake inanyausha mapenzi kama siyo kuyaua kabisa.

6 : Mkiacha kujaliana na kupeana haki katika tendo la ndoa.

Tendo la ndoa ni muhimu kwa wanandoa kwa vile linahusika na hizia za mwili. Matatizo mengi ya usaliti kwa mujibu wa uchunguzi, yanatokana na wapenzi kutotoshelezana wakati wa tendo la ndoa. Kwa kutokutambua madhara au kwa uzembe, wapenzi wengi wamekuwa wakiacha kutimiziana tendo hilo bila kuwepo kwa sababu za msingi. “Mimi nimechoka siwezi kufanya mapenzi.”
Inawezekana kweli mtu akawa kachoka sawa na kauli hiyo lakini sababu hiyo haiwezi kumfanya mwenza akazimaliza hisia zake, isipokuwa kwa kutafuta njia mbadala zikiwepo za usaliti. Sambamba na hilo wapenzi wengi wamenyausha mapenzi yao kwa kutokuwa wabunifu katika uwanja wa sita kwa sita kwa kutokujituma, kutobuni staili mpya, kutochombeza na kutohamasisha kwa cho chote na kibaya zaidi kutokuwepo kwa usafi wa mwili yao.

Katika kipindi cha maisha yangu ya ushauri wa masuala ya saikolojia, maisha na mapenzi nimekuwa nikikutana na wanaume wengi wanaolalamika kuwa wana upungufu wa nguvu kiume. Lakini wengi kati ya hao ambao mamia yao nimeshawasaidia walijikuta wakipungukiwa nguvu zao kwa sababu za kisaikolojia zilizochochewa pia na udhaifu wa wenza wao. Kama utakuwa na mtu kwa mfano, ambaye mtakutana naye chumba kile kile, eneo lile lile, staili zile zile, kwa miaka mitano mfululizo bila shaka hali ya kukinaishwa itakuwepo na hivyo mapenzi kunyauka. Katika hili ni vema kujifunza zaidi namna ya kutoshelezana katika tendo la ndoa.

7 : Mkibeba fikra binafsi kwa kila mtu kutaka mafanikio yake.

Maisha ya wapenzi wengi yamekuwa yakipoteza maana kiasi cha kufikia kuchuja kutokana na wapenzi wenyewe kuwa na mawazo ya ubinafsi. Utakuta watu wameoana lakini kila mmoja anakabili changamoto za maisha peke yake, hali ambayo humfanya atumie nguvu kubwa kutafuta ushindi wa matatizo yake.

Mantiki ya maisha ya ndoa ni kusaidiana. ‘Mungu alimwambia Adamu kuwa atampatia msaidia wa kufanana naye ambaye ni mwanamke aliyeitwa Hawa.’ Upo pia msemo usemao ‘Kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi’ Ni wajibu wa wanandoa kuhakikisha kuwa maisha yao yanakuwa ya nyuzi mbili ili yasikatike upesi. Lakini ikiwa kila mtu anajenga nyumba yake, anafanya biashara zake, ana mipango yake binafsi ujue mwisho mbaya wa mapenzi umesogea.

8 : Mkiwa watu wa kutoa siri zenu nje.

Upo udanyanyifu mwingi wa kimawazo miongozni mwa wapenzi wengi kiasi cha kudhani kuwa kumwambia rafiki au ‘shoga’ masuala ya ndani ya ndoa ni kutafuta suluhu ya matatizo. Hii si sahihi kwa vile upo ushahidi mkubwa juu ya wapenzi wengi ambao walijikuta katika wakati mgumu baada ya kutoa siri zao nje. Ifahamike kuwa ndoa imara ni ile inayoheshimika katika jamii, na heshima hiyo haiwezi kuwepo kama wanandoa hawatakuwa makini katika kutunza siri za mapenzi yao.

Haipendezi kwa mwanamke/ mwanaume kwenda kijiweni na kuanza kuanika mambo ya ndani kwa mfano. ‘Yaani leo mume wangu hakuacha kitu chochote ndani sijui itakuwaje. ‘Sema wanawake wote lakini si mke wangu, ana kasoro nyingi sana.’
Kauli kama hizi na nyingine ambazo zinatoa nje udhaifu wa maisha yenu hazifai, kwani katika kila ndoa kuna udhaifu mwingi ukiwepo ukimya ina maana wahusika wanaweka udhaifu wao kifuani kwa maslahi ya maisha yao. Na wewe uwe hivyo kwa kutunza siri za mumeo.mkeo.

9 : Msipokuwa wawazi katika kuzungumzia upungufu wa kibinadamu mlionao na kusaidiana.

Wapenzi wasomaji wangu, hakuna mwanadamu aliyekamili kwa asilimia mia moja. Ukimuona hodari wa hili ni dhaifu wa lile, kinachotakiwa ni kusaidiana katika kufikia ukamilifu. Faraja inayopatikana katika upungufu wa mwanadamu hasa usiokuwa wa kimaumbile ni kuwepo kwa utatuzi wake. Kuna wapenzi wengi wamefikia kuachana kwa kasoro ndogo ndogo kama za kutojua mapenzi, au hata uchafu wa mwili ambao kama wangekaa na kujadiliana pamoja wangepata ufumbuzi wa tatizo.

Inashauriwa kuwa kunapokuwepo upungufu wowote wa kati ya mwanaume na mwanamke ni wajibu wa wapenzi wenyewe kukaa chini na kuelezana wazi na kushirikiana katika kupata ufumbuzi. Unashindwa nini kuwambia mpenzi wako kuwa hakutoshelezi katika tendo la ndoa, ana harufu mbaya mwilini, mchafu, hajui mapenzi na mambo kama hayo! Kikubwa katika hili ni kujua namna ya kuwasil;isha ujumbe, maana kuna wengine hawana lugha nzuri za mawasiliano “Yaani mke wangu unanuka sana mimi nakerwa sana” Ukisema hivi utamfanya mwenzako aone kama unamnyanyapaa. Tumia lugha nyepesi itakayosaidia kumaliza tatizo msikae kimya bila kuzungumzia upungufu wenu mtajikuta mnaachana.

10 : Mkiendekeza nguvu katika kutwaa madaraka ndani ya familia.

Kuna baadhi ya familia kila mmoja ni mtemi hakuna diplomasia katika kutatua migogoro. Utakuta mwanamke ni mbogo na mwanaume naye ni simba, basi shughuli inakuwa nzito. Ndoa inakuwa uwanja wa ndodi kila siku kutoana manundo. Hakuna mapenzi ya namna hiyo! Kanuni za mapenzi bora zinakataza wapenzi kutumia nguvu kutwaa madaraka au haki ndani ya familia. Inawezekana kabisa wewe kama mke/ mume ukwa na haki katika jambo fulani lakini haki hiyo haikupi fursa ya kutumia nguvu nguvu kuipata.

Kinachotakiwa katika mapenzi ni kuheshimiana, kwani katika hali ya kawaida utumiaji wa nguvu katika kudai haki ndani ya familia ni moja kati ya mambo yaliyoshindwa katika historia kuleta maelewano. Kama unadhani naongopa keti chini ujitathmini tangu umeanza kumchunga mumeo/mkeo na kumbana kwa ngumi umepata mafanikio gani, ameacha tabia yake au ndo anazidi? Umwamba haufai kutumika katika maisha ya ndoa kwa mtu yoyote awe mwanaume au mwanamke.